Gari lagonga mwendesha baiskeli na kusababisha kifo Jijini Mwanza

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja


Mnamo tarehe 11.05.2016 majira ya 13:30hrs mchana katika barabara ya Mwanza – Simiyu eneo la Igoma Kata ya Nyakato Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza, gari namba T. 488 CDZ aina ya Scania Tractor likiendeshwa na dereva aitwaye Enock Mshihiri miaka 24, msukuma mkazi wa Igoma lilimgonga mwendesha baiskeli aitwaye Sanyiwa Nengo miaka 60, msukuma mkazi wa Busekwa na kusababisha kifo chake papo hapo. 
Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa Scania kushindwa kulimudu gari alipokua barabarani. Mtuhumiwa wa ajali hiyo amekamatwa, pindi uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayo mkabili. Mwili wa marehemu upo hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi AHMED Z. MSANGI anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa nipamoja na kufuata na kuheshimu sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. 
Lakini pia anatoa wito kwa watumiaji wengine wa barabara wakiwemo watembea kwa miguu nao wachukue tahadhari pindi wanapokua barabarani.

Imetolewa na:
SACP. AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Bonyeza Like

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI