Kafulila Naye Apigwa Chini kesi Yake Ya Kupinga Matokeo Ya Uchaguzi dhidi Ya Hasna Mwilima mahakama kuu kanda ya Tabora

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja


Mbunge wa zamani wa   Kigoma kusini (NCCR-MAGEUZI), David Kafulila ameshindwa kwenye kesi yake iliyokuwa ikisikilizwa mahakama kuu kanda ya Tabora kuhusu kupinga matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa CCM, Hasna Mwilima
 
Kesi hii ilifunguliwa katika mahakama kuu kanda ya Tabora na kuendeshwa  chini ya Jaji Ferdinand Wambari.
 
Katika kesi hiyo upande wa mlalamikaji (Kafulila) uliongozwa na mawakili Prof. Abdallah Safari, Tundu Lissu na Daniel Lumenyera, Ili hali upande wa mlalamikiwa (Husna) uliongozwa na wakili Kenedy Fungamtama pamoja na mawakili wa serikali upande wa mwanasheria mkuu.

Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Bonyeza Like

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI