Kigogo wa CCM Ataka Maalim Seif Sharif Hamad Akamatwe

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Kigogo wa CCM aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Sukwa Said Sukwa amevishauri vyombo vya dola visiwani Zanzibar kumchukuliwa hatua haraka Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kwa kauli yake aliyoihusisha na kosa la uhaini.

Sukwa aliitaja kauli ya Maalim Seif aliyoitoa alipokuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara kisiwani Pemba kuwa Dk. Ali Mohamed Shein hatamaliza kipindi chake cha urais mwaka 2020 na kwamba ni dikteta.

Sukwa amesema kuwa kauli hiyo ya Maalim Seif haipaswi kupuuzwa hata kidogo kwakuwa kauli kama hizo ni zaidi ya sumu.

“Sivilazimishi vyombo vya dola kufanya ninavyotaka, lakini tunashauri tu visipuuze ushauri wetu kwa sababu ulimi wa mtu unaweza kuwa sumu hatari kuliko matendo yake,” Sukwa aliliambia gazeti la Raia Tanzania.

Maalim Seif amekuwa akifanya mikutano kuwataka wananchi kumuunga mkono kuikataa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Shein, akieleza kuwa uchaguzi wa marudio haukuwa wa haki.

Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Bonyeza Like

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI