Serikali Yasema Kusitishwa kwa Baadhi ya Misaada ya Wahisani Hakujaathiri Sekta ya Nishati

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo ameliambia Bunge Mjini Dodoma kwamba miradi ya umeme vijijini (REA) haijaathirika chochote kwa Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) kuondoa misada yake Tanzania.

Muhongo ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa aliyetaka kujua serikali imepata hasara kiasi gani kwa MCC kuondoa fedha zake katika miradi ya umeme nchini.

Akijibu swali hilo Prof Muhongo amesema fedha za MCC zilikuwa haziendi kwenye miradi ya maendeleo ya umeme vijijini hivyo miradi hiyo itaendelea kama ilivyopangwa.

''Hakuna dola hata moja ya MCC iliyokuwa inaenda kwenye umeme vijijini fedha zilikuwa zikienda kwenye miradi ya maji, barabara na nishati lakini siyo umeme wa vijijini na fedha za kwenye nishati zilikuwa hazivuki theluthi moja hivyo kama umejiandaa kulima hekari 8 akakuongezea mtu 2 ili zifike 10 siku akiondoa za kwake utandelea na zako 8 kama kawaida''- Amesisitiza Prof. Muhongo.

Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) ilisema Tanzania haijatimiza viwango vinavyohitajika ili kunufaika na ufadhili kutoka kwa shirika hilo, na hivyo basi haitapokea msaada wa awamu ya pili ambao ulikuwa wa jumla ya Dola 472.8 milioni ambazo ni sawa na shilingi trilioni moja za Tanzania.

Kwa awamu ya kwanza Tanzania ilipokea Dola 698 milioni na moja kati ya mambo yaliyosababisha MCC kuondoa fedha zao ni pamoja na kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar.

Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Bonyeza Like

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI