Huu Hapa Ndio Ujumbe Mzito Uliopostiwa Na Lowassa Leo

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja


Nina furaha kutimiza mwaka mmoja toka nilipojitoa CCM na kujiunga na CHADEMA.Uamuzi ule haukuwa rahisi,lakini kwa ushupavu, ujasiri na mwongozo wa Mungu nilifanya hivyo.Nilifanya uamuzi wa kihistoria katika nchi yetu.

Najivunia kwa uamuzi ule,kwani umewafungua macho watanzania wengi na kuimarisha demokrasia.Nimeingia CHADEMA nimewakuta viongozi na wanachama waliyo na moyo wa dhati wa kuliletea ma
endeleo taifa lao KIVITENDO.Najihisi mwenye furaha kubwa na raha kuwa katika upande huu.

Watanzania bado wanataka mabadiliko na imezidi kuthibitika kuwa hawawezi kuyapata ndani ya CCM .Watanzania wanataka sera na mtu mbadala wa kuongoza mabadiliko hayo.Vyote hivyo watavipata ndani ya CHADEMA na UKAWA kwa jumla.

Nawahakikishia watanzania na wana UKAWA kwa jumla,kuwa sasa hivi NINA ARI,NGUVU NA HAMASA kubwa kuliko wakati mwengine wowote.

Kwa wale wenzangu waliyobaki CCM na wanaoniunga mkono,tuendelee kushikamana na kunipatia taarifa kwa hatma ya nchi yetu.Nawashukuru watanzania kwa kuendelea kuniunga mkono mimi na wenzangu ndani CHADEMA.

Edward Ngoyai Lowassa
Mjumbe wa kamati Kuu CHADEMA
Waziri Mkuu mstaafu

Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Bonyeza Like

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI