USHIRIKINA !! Kijana Anasa Mlangoni Kwa Bibi Anayedaiwa Kumchezea Kishirikina Usiku Kucha

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja


Katika hali isiyo ya kawaida Mkazi wa Mtaa wa Majengo wilayani KAHAMA Mkoani Shinyanga aliefahamika kwa jina moja la MLINDA amekutwa amenasa katika mlango wa nyumba ya Bibi mmoja mtaani hapo, tukio linalohusishwa na imani za kishirikina.

Akizungumza na Dunia Kiganjani Blog Balozi wa eneo la MAJENGO Stendi Ndogo HELENA JOEL amesema baada ya kufika eneo hilo jana alimkumkuta kijana huyo amesimama mlangoni na kushindwa kutoka.
 
Kwa upande wake VASHTINI TIMBA amesema kwa mujibu wa maelezo ya watu ni kwamba MLINDA alienda nyumbani kwake na akaanza kujiskia vibaya ndipo alipo amua kurejea sehemu alipokuwepo awali ambapo ni nyumbani kwa bibi huyo.
 
Jeshi la polisi wilayani Kahama limekiri kufika eneo la tukio na kumtoa MLINDA na hadi sasa yupo hospitali ya wilaya ya Kahama.

Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Bonyeza Like

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI