Mrema amtaka Lowassa akubali kwamba alishindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Mwenyekiti wa Bodi ya Parole ambaye pia ni Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema amemtaka Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akubali kwamba alishindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na akae kimya hadi mwaka 2020.

Mrema aliyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam na kusisitiza kwamba alimtaka Waziri Mkuu Mstaafu watoke CCM pamoja kwa kuwa nguvu ya upinzani ilikuwa kubwa sana.

‘’Mimi nitamuuliza 1995 wakati natoka nilikuambia tutoke sasa maji yamechemka tukiweka unga tutakula ugali ukagoma, ukasema unaendelea kula kidogo hadi alipojiuzulu akaendelea na CCM hadi alipotaka kugombea Urais akakataliwa na wenzake ndipo akaja upinzani’’

Mrema aliongeza kwamba Chama cha Mapinduzi kilitakiwa kuondoka madarakani mwaka 1995 ambapo yeye ndiye alikuwa na nguvu kubwa ya kisiasa nchini.

Aidha Mrema amewataka vijana kuwa makini na upinzania kwa kuwa Lowassa alijiunga na upinzani baada ya kunyimwa nafasi ya kugombea Urais ndani ya CCM hivyo wajiepushe na maandamano kwani hayana faida kwao.

Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Bonyeza Like

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI