Uchawi Ni Utumwa : Nilimlisha Mume Wa Mtu Limbwata La Nyama Ya Bundi- Sehemu Ya Pili

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

SEHEMU YA PILI….

NASHIRIKI KUMFUNGA KICHAWI MUME WA MTU….
Katika makala yangu yaliyopita , nilieleza jinsi mungu wa kabili alivyo niambia kuwa nina nyota ya uganga na hivyo ninatakiwa kusimikwa uganga.


mungu wa kabili aliniambia ili nifundishwe uganga ni lazima nianze kufundishwa kuhusu uchawi kwanza, kwa sababu kazi yangu kubwa katika uganga itakuwa ni ' kupambana na uchawi ". ( NI UNAFIKI MKUBWA KUSEMA ETI MGANGA ANAPAMBANA NA UCHAWI, KWA SABABU MGANGA NA MCHAWI LAO NI MOJA, NA SIKU ZOTE HUSHIRIKIANA ...KADRI UNAVYO FUATILIA WARAKA WANGU NDIPO UTAKAPO GUNDUA UNAFIKI WA WAGANGA KUHUSU HOJA HII DHAIFU ).


mungu wa kabili aliniambia ni lazima nianze kwanza kwa kupewa elimu ya msingi ya uchawi kabla ya kufundishwa uganga na hatimaye kusimikwa uganga rasmi.


Nilifundishwa mambo mengi sana ya kichawi na katika mfululizo wa makala haya nitayaelezea yale muhimu na ninayo yakumbuka vizuri.


Lengo langu ni kuwafungua watu macho kuhusu ulimwengu wa wachawi, jinsi unavyo fanya kazi na jinsi unavyo weza kujikinga ama kujiepusha nao.


Vile vile lengo langu ni kuwaonyesha watu jinsi uchawi unavyo wafanya watu kuwa watumwa katika maisha yao ya kila siku..


NAFUNDISHWA UCHAWI WA KUPIGA MAFUNDO AMA KUFUNGA MAFUNDO...
Huu ni aina ya uchawi ambao kila mchawi hufundishwa. Ni uchawi unao tumika sana miongoni mwa wachawi.


Uchawi wa kufunga mafundo ni uchawi unao fanyika kwa ajili ya kuwafunga watu katika vifungo vya aina mbalimbali, kama vile kutokuzaa, kutokuoa ama kuolewa, biashara kutokufanikiwa, mtoto kutokukua, nakadhalika.


Uchawi huu unaweza kufanyika kwa lengo la kumkomoa na kumtesa mfungwaji , kumshinikiza mfungwaji au kumfurahisha na kumstarehesha mfungaji.


MAMBO MAKUU MATATU MUHIMU KATIKA UCHAWI WA KUPIGA MAFUNDO.


Katika uchawi wa kupiga mafundo ama uchawi wa kuwaweka watu kwenye vifungo mbalimbali, kuna mambo makuu matatu ya msingi.


JAMBO LA KWANZA NI MFUNGAJI ( Yaani mtu aliekusudia kumfunga mwenzake kichawi )


JAMBO LA PILI NI MFUNGWAJI ( Yaani mtu alie kusudiwa kufungwa )


JAMBO LA TATU NI KIFUNGO CHENYEWE. ( Yaani jambo au kitu ambacho kitatumika kumfunga aliye kusudiwa kufungwa )


Nitaelezea kwa ufupi jambo moja hadi jingine. Naanza na jambo la kwanza ambalo ni MFUNGAJI.


MFUNGAJI NI NANI KATIKA UCHAWI ? Katika uchawi mfungaji ni mtu alie kusudia kumfunga mtu mwingine kichawi. Mtu huyu anaweza kuwa mchawi ( mlozi), mganga ( ambae pia ni mchawi ), jini, pepo, mzimu au mtu mwingine yoyote ambaye si mchawi wala mganga ambaye ameenda kwa mchawi ama mganga, kwa ajili ya kutafuta msaada wa kichawi wenye lengo la kumfunga kichawi mtu mwingine..


MFUNGWAJI : Mfungwaji ni mtu aliye kusudiwa kufungwa na mfungaji. Mfungwaji ni ni jambo au hali yoyote iliyo kusudiwa kufungwa na mfungaji. Mfungwaji ni jini, pepo au mzimu wowote ulio kusudiwa kufungwa na mchawi. Mfungwaji ni mnyama, mmea au mali yoyote iliyo kusudiwa kufungwa na mfungaji.


Mfungwaji anaweza kuwa mume wa mtu, mke wa mtu, mtoto mchanga, mchungaji, padre, imamu, mimea, mazao au kitu chochote kile unacho weza kukifi9kiria.


KIFUNGO CHA KICHAWI : Katika ulimwengu wa wachawi, kifungo ni ile hali au jambo ambalo limekusudiwa kwa mfungwaji. Hali au jambo hilo laweza kuwa ugumba, utasa, mimba kutoka, kifo, biashara kushindwa, chuma ulete, mapenzi, undondocha, umalaya, ukichaa, uwehu nakadhalika...


Pia kifungo huusisha KAMBA ZA KICHAWI ama KAMBA ZA KUZIMU.


Hivyo basi ili kifungo cha kichawi kiweze kufanya kazi ni lazima, awepo mfungaji, mfungwaji na kifungo chenyewe...


JINSI WATU WANAVYO WAFUNGA KICHAWI WATU MBALIMBALI..
Nikiwa kama mwanafunzi wa mungu wa kabili, nimeshiriki katika kuwafunga kichawi watu mbalimbali.


Katika ulimwengu wa wachawi, binadamu amegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni MWILI, NAFSI NA ROHO.
Kwa lugha nyingine, wachawi wana amini kuwa mwanadamu ni roho yenye nafsi ambayo inaishi kwenye nyumba ya udongo iitwayo mwili.
Hivyo basi mfungaji anapotaka kumfunga mtu kifungo anatakiwa kuelewa anataka kumfunga mtu huyo kifungo cha wapi. Cha mwili, nafasi au roho ?


KIFUNGO CHA MWILI : Wachawi wana amini kuwa mwanadamu aliumbwa kwa udongo. Hivyo basi wanapotazama mwanadamu katika macho ya kiroho humuona kama udongo kabisa.


Na kwa kuwa binadamu kwao ni udongo, basi wachawi wanaweza kkutumia maarifa ya kichawi kupanda chochote katika mwili wa mwanadamu na kitu hicho kikakua na kuota.


Katika ulimwengu wa wachawi, kinacho ongeza thamani ya mwili wa mwanadamu, ni mapando yaliyo pandwa katika mwili wa mtu huyo.


Aina ya vitu vilivyo pandwa kwenye mwili wako, ndio itakayo amua, aina ya kifungo utakacho fungwa.


Kama mwili wako ni mweupe, basi utafungwa kifungo cha kawaida, na kama katika mwili wako, imepandwa ngome imara basi hata nguvu ya uchawi itakayo tumika itakuwa kubwa zaidi.


Ukisikia mchawi anakwambia nipe jina la mama wa mtu unayetaka kumroga basi jua anataka kutazama mwili wa mtu huyo umepandwa kitu gani...


Ukisikia mtu ni mzito katika uchawi basi jua mwili wake umepandwa vitu vizito pia.


JINSI WACHAWI WANAVYOPANDA MAPANDO MBALIMBALI KWENYE MWILI WA MWANADAMU..


Wachawi hupanda mapando mbalimbali katika mwili wa mwanadamu kwa kutumia njia mbalimbali, mojawapo kati ya njia hizo ni pamoja na kuchanjwa, kuogeshwa dawa pamoja na kulishwa dawa.


Njia nyingine wanatumia migomba, udongo na mti mmoja wa porini ambao jina lake silikumbuki vizuri.


Kwa kutumia maarifa ya uchawi, wachawi wanaweza kupanda kitu chochote wanacho jisikia katika mwili wa mtu walie mkusudia.


SHUHUDA ZA WATU WALIO FUNGWA VIFUNGO MBALIMBALI KICHAWI....


Kwa muda wa miaka mitatu na ushee ambao nimekuwa nikifanya kazi kama mwanafunzi wa uchawi wa mungu wa kabili, nimeshiriki katika kuwafunga kichawi watu mbalimbali. Zifuatazo ni baadhi ya shuhuda za watu ambao nilishiriki katika kufungwa kwao.


NASHIRIKI KUMFUNGA MWANAUME KICHAWI ….
Kuna mwanamke mmoja tajiri na mwenye uwezo mkubwa tu kifedha, alileta kesi kilingeni kwa mungu wa kabili. Kesi ilikuwa hivi, yeye alikuwa amefunga ndoa na mwanaume asiye na kipato, lakini mwanaume alikuwa si muaminifu katika ndoa .


Mapenzi yalikuwa ya upande mmoja. Mwanamke alikuwa anamudumia mwanaume kwa kila kitu lakini mwanaume alikuwa haridhiki. Na mpaka mwanamke huyo anafika kilingeni kwa mungu wa kabili, mwanaume alikuwa ameondoka kwa mwanamke ( walikuwa wanaishi kwenye nyumba ya mwanamke ) na kwenda kuishi kwa mwanamke mwingine kwa zaidi ya miezi minane. Mwanaume huyo aliondoka baada ya kutokea ugomvi mkubwa kati yao, chanzo kikiwa ni wivu wa kimapenzi. Mwanamke alikuwa akimtuhumu mwanaume kwa kutoka nje ya ndoa.


Mwanaume huyo alikuwa amempa ujauzito mwanamke huyo wa pembeni. Mwanamke huyo wa pembeni nae alikuwa na uwezo wa kifedha.


Mwanamke alikuwa anaomba kusaidiwa, ufanyike uganga, huyo mwanaume arudi mwenyewe nyumbani, na atakapo rudi nyumbani atulie na kumuheshimu mke wake. Pili watenganishwe mwanaume huyo na mwanamke wake wa pembeni, mimba ya mwanamke huyo itolewe na mwisho mwanamke huyo atiwe mikosi


Mungu wa Kabili akaagiza vipatikane vitu vifuatavyo : Kamba ambayo mtu ametumia kujinyonga, nguo za marehemu ambazo alikufa nazo, kipande cha sanda ambacho kimekatwa kutoka kwenye sanda iliyo valishwa mwili mwa marehemu, mchanga wa njia panda saba, sindano arobaini, shahidi la kaburini pamoja na udongo wa kaburi alilozikwa mwanaume, maji yaliyo tumika kuoshea maiti ya mwanamke, kamba iliyo tumika kumfunga kondoo, mafuta ya msukule, yai la bundi, jani lililo letwa lenyewe na upepo na likadakwa kabla halijafika chini, kondoo, punda mwenye alama ya msalaba mgongoni, bundi wa kichawi, kobe wa kichawi ( Hapa naomba nifafanue jambo;, wachawi huwa wana namna yao ya kuwaita majini walio katika maumbo ya wanyama, ndege na wadudu mbalimbali. Ukisikia mnyama wa kichawi basi jua huyo sio mnyama wa kichawi bali ni jinni amegeuzwa na kufungwa katika umbo la mchana ) , maji yaliyo tumika kuchambia sehemu za siri za mwanamke ambayo yanatakiwa yaletwe na mwanamke mwenyewe, maji ya kwanza ambayo mwanamke ameyatumia kunawia uso, funza walio nyonya damu ya maiti ya binadamu , funza wa bundi pamoja na unyayo wa mwanaume huyo akiwa anaingia ndani na sio akiwa anatoka.


Mungu wa kabili akaagiza pia wapatikane njiwa wawili jike na dume, ndege wawili wa porini ambao sifa zao zipo hivi, ukimkamata ndege huyo na kumfunga kwa kamba sehemu yoyote ile, iwe ni porini huko huko au kwenye banda, kesho yake asubuhi utakuta kamba imejifungua na ndege ondoka, katika jamii ya ndege hawa, dume huwa dogo kwa umbo kuliko jike, na dume ndio huatamia mayai.


Ndege hawa, wana macho mekundu na mkia mrefu, na ukucha wa kidole kikabilicho nyuma ni mrefu sana . Ndege hawa wana mabawa ya kahawia nyekundu na kichwa chenye rangi nyeusi.


Chakula kikuu cha ndege hawa ni wadudu, mijusi, nyoka na wanyama wadogo, mayai ya ndege na wadufu mbalimbali, makinda ya ndege mbalimbali, matunda na mizoga pia.


Vichali vya ndege hawa hujengwa kwenye eneo lenye miti mingi na hufungwa kwa juu.


Kuna mnyama mmoja anapatikana porini. Chakula kikuu cha mnyama huyo ni asali. Ana sifa ya kuwa na makucha marefu na yenye nguvu sana. Huwa anaishi peke yake porini katika shimo ambalo anakuwa amelichimba yeye mwenyewe…


Na anapochimba shimo lake, hukaa ndani ya shimo hilo kwa muda wa dakika kumi tu.


Jino la mnyama huyu hutumiwa na wachawi katika kutengeneza dawa ya bahati nasibu.Yani kama unacheza bahati nasibu ama unaenda kwenye ushindani wowote ule iwe ni michezo, kazi, uongozi nakadhalika, halafu ukachanjwa dawa iliyo tengenezwa kwa kutumia jino la mnyama huyo basi, lazima utashinda hata kama mnaogombania nafasi hiyo mpo elfu kumi na anae hitajika ni mtu mmoja.


Dume la mnyama huyu huwa na wivu sana kwa jike lake, na mara nyingi hutembea nyuma ya jike huku akiwa ameziba sehemu za siri za jike huyo. Basi ikitokea hata jani likigusa kwa bahati mbaya sehemu za siri za jike la dume la mnyama huyo, litararuliwa na kupigwa vibaya sana na mnyama huyo.


Mungu wa Kabili akaagiza apatikane mnyama huyo, jike pamoja na dume lake. Pamoja na udongo wa kwenye shimo lilitumiwa na mnyama huyo.


Vitu vingine mungu wa kabili akasema, wapatikane njiwa wawili jike pamoja na dume.


Kazi nyingi za Mungu wa Kabili huwa anazifanya nyakati za usiku na huzifanya kwa kushirikiana na watu wanaoitwa malaika wa mungu wa kabili. Hawa malaika wa mungu wa kabili, ni wachawi wazito wazito.


Malaika wa mungu wa kabili wapo karibu katika kila kona ya nchi hii na nchi jirani, hususani Kongo .


Ndio maana ninasisitiza kwamba, mungu wa kabili ni mchawi na wakala wa shetani.


Kabla sijaendelea, naomba nifafanue kitu kimoja, kwamba waganga wapo wa aina kuu mbili, aina ya kwanza ni wale wanao agua kwa njia za kawaida tu, na aina ya pili ni ile ya waganga wanao agua kichawi.


Mungu wa Kabili ni mganga anae agua kichawi, na ndio maana kazi zake nyingi hufanyika nyakati za usiku na huzifanya kwa kushirikiana na wachawi…


Mungu wa Kabili alisema kamba ambayo mtu ametumia kujinyonga, nguo aliyo kufa nayo marehemu, jani lililo letwa lenyewe na udongo wa kwenye shimo alilo tengeneza mnyama niliye muelezea hapo juu, shahidi la kaburi , udongo wa kaburini pamoja na kipande cha sanda kilicho katwa kutoka kwenye sanda iliyo tumika kumfunika marehemu, hutumika katika kutengeneza uchawi wa kumuita ama kumvuta mpenzi au mtu yoyote aliye kimbia.


Kamba iliyo tumika kumfunga kondoo, hutumika katika kutengeneza uchawi wa kumfunga mume, mke , mchumba, mfanyakazi nakadhalika.


Kobe wa kichawi hutumika katika kutengeneza uchawi wa kumuinamisha na kumfunga na kumtuliza mume au mke. Mke au mume aliye fanyiwa uchawi huu, huwa ni mtu wa kuwa ndani wakati wote, akitoka nje basi labda kaenda kazini, hospitali, kanisani,msikitini au msibani.


Bundi wa kichawi hutumika kutengeneza uchawi wa kumlisha mwanaume na kumfanya kuwa mtumwa wa mwanamke wake katika siku zote za maisha yake.


Maji yaliyo tumika kuoshea maiti, funza walio nyonya damu ya maiti ya mtu au maiti ya msukule, hutumika katika kutengeneza uchawi wa kumfanya mke au mume akupende wewe peke yako tu, na awe sawa sawa na mtu aliye kufa na kuoza juu yako.


Uchawi huo humfanya mtu aliyefanyiwa kama ni mwanaume, basi asikumbuke chochote kuhusu mwanamke au mke aliye kuwa nae kabla, hadi siku atakayo kuwa anaingia kaburini ndio atakumbuka kumbe alikuwa amemuoa mwanamke Fulani. ( NDUGU ZANGU, MKIONA AU KUSIKIA MWANAUME AMA MWANAMKE KAIKIMBIA NA KUISAHAHU FAMILIA YAKE, BASI JUENI KUWA AMEFANYIWA UCHAWI WA AINA HII . MUNGU AWAEPUSHIENI MBALI NA USHETANI HUU. NI HATARI SANA )


Mafuta ya msukule yana matumizi mengi sana katika uchawi, katika habari ya ulozi wa mapenzi hutumika katika kumfanya mke, mume,mchumba, boyfriend au girlfriend asionekane na watu wengine..


Haya mafuta ya msukule ni tofauti na mafuta ya usiku. Mafuta ya usiku ni mengine na mafuta ya msukule ni kitu kingine.


Pia mafuta ya msukule ni tofauti na maji ya msukule. Mafute ya msukule yanatengenezwa usukuleni, ilihali maji ya msukule yanatoka kuzimu.


Kuzimu kuna mito saba. Kila mto una matumizi yake. Kati ya mito hiyo, upo mto ambao maji yake yana tumika katika kuwafanya watu wasahahu kila kitu walicho kuwa wanakifahamu kabla hawajanyweshwa maji hayo.


Maji hayo hutumiwa na watu wanao chukua watu misukule. Msukule anapo chukuliwa hunyweshwa maji hayo. Na mara tu anapokunywa maji hayo, husahau kabisa kila kitu alicho kuwa ana kifahamu. Husahau kama Alisha wahi kuwa na maisha mengine, husahau kama alikuwa na wazazi, ndugu, jamaa, marafiki nakadhalika.


Ndio maana basi wachawi wakishamchukua mtu msukule, mara baada ya ndugu zake kufanya


“ mazishi hewa “ wachawi humpeleka mtu huyo hadi katika nyumba aliyokuwa anaishi pamoja na nyumba wanapoishi ndugu zake na kumuonyesha ndugu zake… Asipo watambua ndugu zake, basi wanashangilia kwamba, ule uchawi wao umefanya kazi.


Hapa sizungumzii hayo maji ya msukule, ninazungumzia mafuta ya msukule ambayo hutengenezwa usukuleni.


Kujua kama mafuta hayo ni msukule, ukijipaka basi hata kwenye kioo huwezi kujiona.


Tulianza kwa kufanya zoezi la kwanza, ambalo ni kutengeneza uchawi wa kumuita mume wa Yule mama, ambapo mama Yule alipewa dawa hizo na kwenda kuzitumia kumuita kichawi mume wake.


Baada ya mume kurudi nyumbani, mama Yule alifanya kama ali vyo agizwa, yani kuchota mchanga wa mahali alipo kanyagia mume wake wakati anaingia nyumbani hapo.


Hivyo mama Yule alikuja na mchanga alio mchota mume wake, maji ya kwanza aliyo tumia kuoshea uso wake, maji aliyo tumia kuoshea sehemu zake za siri, sindano arobaini pamoja na njiwa wawili jike na dume.


Maji aliyo tumia kuoshea uso wake kwa mara ya kwanza, yalichanganywa na dawa zingine kwa ajili ya kutengeneza uchawi wa kumfanya mwanaume wake awe anamuona yeye tu, njiwa wawili jike na dume ( wapenzi ) walichinjwa kwa tambiko maalumu, wakapasuliwa, mioyo yao ikachukuliwa ikawekwa kwenye chungu na kukaushwa pamoja na dawa nyingine kama saba hivi za kichawi, ambazo mume hulishwa na kumfanya kuwa muaminifu kwa mke wake, na mke akilishwa basi nae huwa muaminifu kwa mume wake.


Sehemu iliyo baki kwa mwili wa njiwa nayo ilitumika kupikwa pamoja na maji yaliyo tumika kuoshea sehemu za siri za mwanamke huyo pamoja na dawa nyingine nyingi za kichawi, ambazo zingetumika kumyweshwa na kumuogesha mwanaume.


Baada ya zoezi hilo la kwanza kukamilika, lilibaki zoezi la pili ambalo ni kumfunga mwanaume kwa mke wake, zoezi la tatu ni kumtenganisha mume na mwanamke wake wa pembeni, zoezi la nne ni kutoa ujauzito wa mke wa pembeni mwa mwanaume huyo, zoezi la tano ni kumtia mikosi mwanamke huyo.


ZOEZI L A KUMFUNGA MTU KICHAWI.
Zoezi hili lilifanyika njia panda kuanzia saa sita kamili usiku. Zoezi hilo tulilifanya mimi, mungu wa kabili, mwanamke aliye taka kumfunga mwanamke mwenzake, wasaidizi watatu wa mungu wa kabili pamoja na kikundi cha wachawi wapato arobaini.


Zoezi lilifanyika njia panda iliyokuwa imezungukwa na moto wa kichawi ambao wao wachawi wanauita chenge.


Mungu wa kabili aliniambia, zoezi la leo litakuwa zito kidogo kwa sababu, tuna kazi nyingine kubwa ya kumfanya mtu asionekane duniani.


Kwa hiyo tutaanza na kazi ya huyu mama, halafu tukimaliza hapo tutaendelea na kazi nyingine. Ninataka ujifunze kuhusu uchawi wa namna ya kumfanya asionekane duniani.


Kwanza tulifika njia panda, majira ya saa sita kamili za usiku. Tulikuwa mimi, mungu wa kabili, mama mwenye kutaka kumfunga mume wake, pamoja na wasaidizi watatu wa mungu wa kabili.


Wote tulikuwa tumevaa mavazi wanayo vaa wachawi wanapo enda kuroga pamoja na kupakwa unga.


Mungu wa kabili alisema, ataanza kwa kuwaita kwanza wachawi, watakapo fika ndio tutaanza kazi yetu.


Akasema lakini kabla ya zoezi la kuwaita wachawi kufanyika, nitaanza kwa kuchanjwa dawa itakayo nipa uwezo wa kuwaona wachawi….


Kuna mti mmoja, unapatikana porini, mti huo ukikomaa, urefu wake hauzidi wa mtoto wa miaka saba, una magamba kwa mbali na rangi yake ni nyeupe.


Mti huu ukikauka ukausaga unga wake huwa mweupe kama mti wenyewe.


Ukichukua unga wa mti huu halafu ukajipaka usoni unakuwa na uwezo wa kuwaona wachawi.


Ukichanjiwa mti huu kwenye pande saba za mwili wako, ukijipaka unga wa mti huu usoni halafu ukatembea mtaani wakati wa mchana, unaweza kuona mambo yote yanayofanyika katika siri kubwa kama vile wachawi wakiwa wanawanga au wanafanya shughuli zao wakiwa uchi.


Mti huu unakupa uwezo wa kuwaona misukule.


Vilevile mti huu unauwezo wa kukimbiza nyoka mfano ukiwa na kipande cha mti huu


mfukoni au ukiwa umechanjiwa mti huu halafu ukawa unatembea, kama mbele yako kuna nyoka atakimbia kabla hujafika.


Hata ukikaa mahali kama kuna nyoka hawezi kukaa hapo, atakimbia tu…


Mungu wa Kabili alianza kwa zoezi la kunichanja katika pande saba za mwili wangu,na kunipakaa unga wa mti huo, pamoja na kunipaka mashavuni, kidevuni na usoni.


Baada ya zoezi hilo kukamilika, Mungu wa Kabili, alisema maneno yake ya kiganga halafu akaanza kupuliza FILIMBI YA KICHAWI.


Naomba nifafanue kitu kimoja hapa, FILIMBI YA KICHAWI, hutengenezwa kwa kutumia UUME WA MTOTO MDOGO na wapokosa uume wa mtoto mdogo, hutumia hata uume wa mtu mzima,lakini kipaumbele chao huwa ni uume wa mtu mzima.


Sharti moja la kuchukua uume kwa ajili ya kutengenezea filimbi ya kichawi, huwa ni lazima mtoto huyo awe hai, kamwe uume hauchukuliwi mtoto akiwa amekufa, bali unachukuliwa mtoto akiwa hai na huchukuliwa kichawi.


Jinsi wanavyo chukua uume wa mtoto kichawi, huuchukua na kuubadilisha na kipande cha mgomba wa ndizi. ( WACHAWI WANA AMINI, MTI WA MDIZI UNA UHUSIANO WA KINASABA NA BINADAMU.. NA UNAFANANA SANA NA BINADAMU, KUANZIA MFUMO WA NGOZI, UZAZI NAKADHALIKA, NITALIELEZEA KWA KINA SIKU ZIJAZO )


Kuna mti mmoja unapatikana porini, mti huu ni miongoni mwa miti mikuu ya wachawi, una matumizi mengi ikiwa ni pamoja na kupasua makaburi kuongea na mizimu.


Lakini pia mti huu unatumika kuhamisha vitu kutoka katika sehemu moja ya mwili wa mtu kwenda katika sehemu nyinginezo za mwili wa mtu huyo, au kutoka kwenye mwili wa mtu huyo kwenda kwa mnyama, ndege, mdudu, kaburini, pangoni n.k, au kutoka kwa mnyama, mdudu, mmea, eneo n.k kwenda kwa mwanadamu.


Kwa mfano siku moja kuna mama mmoja mtu mzima, ambaye ni mwana ukoo wa mungu wa kabili, aliletwa kilingeni kwa mungu wa kabili kwa ajili ya kutibiwa. Yeye alikuwa na kidonda maeneo ya sehemu zake za siri. ( Kwenye kalio ).


Kwa mujibu wa mila na desturi za Tanzania, mungu wa kabili asingeweza kumuona mama huyo akiwa uchi ili amtibie, hivyo alicho kifanya ni kuhamisha kidonda cha mama huyo kutoka makalioni kwenda mkononi , akakitibu kwa kutumia dawa inaitwa mruturutu pamoja na dawa nyingine kama aina kumi na mbili na kukifunga.. Baada ya siku kadhaa kidonda kilicho hamishiwa mkononi kikawa kimekauka na baada ya kukauka kidonda cha mkononi basi na cha makalioni kikawa kimekauka.


Siku nyingine aliletwa mtoto mdogo na wazazi wake akiwa ameshikwa na homa kali sana, tatizo la mtoto huyo ambaye umri wake ilikuwa ni kama miaka miwili na nusu hivi, alikuwa hataki kunywa dawa, hata kulazimisha. Tulipojaribu kumlazimisha akawa anauma meno. Kujaribu kumminya mdomo, ili aachame akatuzi nguvu kwa sababu tulikuwa tunamminya kwa tahadhari, vinginevyo tungeweza hata kumvunja shingo.


Baba wa mtoto akawa amepanick anajua atampoteza mtoto wake. Alivyo kuja mungu wa kabili, kwa kutumia ule mti wa kuhamisha vitu, akahamisha homa ya Yule mtoto kwa baba ake na kuanza kumpa dawa baba yake, baba mtu alivyopata nafuu, basi mtoto nay eye akawa amepona..


Hivyo basi, wachawi wanapotaka kuchukua uume wa mtoto kwa ajili ya kutengeneza filimbi za kichawi, hutumia mti huo, kubadilisha uume wa mtoto huyo na kipande cha mgomba wa ndizi. Na inapotokea hali hii, mtoto huyo huwa hanithi, kwa sababu uume wake unakuwa umechukuliwa msukule,unatumiwa na watu wengine huko.


Tofauti kati ya watu wazima na watoto wadogo ni kwamba, uume wa watoto wadogo, huchukuliwa kwa ajili ya kutengeneza filimbi za kichawi, wakati uume wa watu wazima, hubadilishwa kwa sababu nyinginezo kama vile, kutoa adhabu kwa muhusika nakadhalika.


Basi , muda mfupi baada ya Mungu wa Kabili kupiga filimbi yake ya kichawi, lilijitokeza kundi la wachawi ambao idadi yao inaweza kufika arobaini au zaidi.


Baadae nikaja kugundua kuwa , wachawi hao walikuwa wametumwa na mungu wa kabili kumletea vitu mbalimbali, kama wale funza walio nyonya damu za maiti na damu za maiti za misukule, mafuta ya misukule, wale wa wanyama na ndege nilio wataja hapo juu nakadhalika.


Wachwai walipo fika katika eneo hilo, walisema “ Mkuu Tumeitikia wito wako, na tumefanya kama ulivyo tuagiza “.


Baada ya hapo kila mmoja akaonyesha vitu vyote alivyo agizwa nakadhalika.


Vilianza kutolewa vifaa vya kazi ( ambao wao wachawi wanaviita vizimba ) kwa ajili ya kazi ya kumfunga mume wa Yule mama.


Vitu hivyo vilipikwa kichawi kisha mama Yule akakabidhiwa huku akipewa maelekezo ya kwenda kufanya.


Alipewa dawa za kwenda kumlisha mwanaume Yule, kumuogesha pamoja na kumfunga. Nilicho kisikia baadae ni kwamba, mwanaume Yule aligeuka na kuwa kama zezeta kwa mama Yule.


Baada ya zoezi la kumfunga mwanaume Yule kukamilika, lilifuatia zoezi la kumtenganisha na mwanamke wake wa pembeni. Kuwafanya wasikutane tena hadi siku wanaingia kaburini.


Katika zoezi la kuwatenganisha mwanaume Yule pamoja na mwanamke wake wa pembeni, zilichukuliwa nyayo za Yule mwanaume, pamoja na nyayo za mwanamke wake wa pembeni ambazo zilipatikana kichawi. Lilitumwa jinni kwenda kuchukua nyayo za mwanamke huyo ambazo tayari tulikuwa nazo kabla ya kwenda kuroga.


Nyayo za mwanaume huyo zilichukuliwa na kwenda kufungwa kichawi kwenye mlima mmoja ambao hutumiwa sana na wachawi. Na nyayo za mwanamke wake wa pembeni zilichukuliwa na kwenda kufungwa kichawi kwenye mlima mwingine ambao nao pia hutumiwa sana na wachawi.


Maneno yaliyokuwa yakitamkwa wakati tunafunga na kuzika zile nyayo kwenye hiyo milima yalikua ni pamoja na :


“ WEWE ( JINA LA MWANAUME ) SIKU YA LEO, NIMEKUTENGANISHA NA ( JINA LA MWANAMKE). HADI SIKU YA KUFA KWENU. WEWE ( MWANAUME) PAMOJA NA WEWE (MWANAMKE ) HAMTAONANA WALA KUONANA SEHEMU YOYOTE ILE DUNIANI, HADI SIKU MNAINGIA KABURINI.


KAMA AMBAVYO W EWE MLIMA ( JINA LA MLIMA ) HAUWEZI KUKUTANA NA MLIMA ( JINA LA MLIMA ), BASI VIVYO HIVYO. WEWE ( JINA LA MUME ) PAMOJA NA WEWE ( JINA LA MKE) HAMTAKAA MKUTANE KATIKA SIKU ZOTE ZA MAISHA YENU.


LAKINI KAMA WEWE ( JINA LA MLIMA ) NA W EWE ( JINA LA MLIMA ) MNAWEZA KUKUTANA, BASI HATA ( JINA LA MWANAUME ) NA ( JINA LA MWANAMKE ) WANAWEZA KUKUTANA.


Uchawi huu ulisindikizwa na tambiko la kuchinja mnyamna anaepandwa na mwanadamu.


Ndugu msomaji, usiombee kufanyiwa uchawi huu. Maana hata kama imekusudiwa wewe na mama yako mzazi msionane, basi hamtaonana mpaka siku mnaingia kaburini.


Baada ya zoezi hili kufanyika, lilifanyika zoezi la kutoa kichawi ujauzito wa mwanamke wa pembeni wa mume wa Yule mama aliye leta mashitaka kwa mungu wa kabili.


Mungu wa Kabili alichukua yai moja la bundi ya yai moja la kuku. Kwanza akachukua fimbo yake ( ile ya kubadilisha vitu ), akainyoosha juu, halafu akaipiga ardhini kisha akaigusa gusa kwenye tumbo la Yule mama,. Alifanya hivyo kama mara saba hivi.


Baada ya hapo alichukua lile yaio la bundi, akalisugua kwenye tumbo la Yule mama kama mara saba tena.


Alipomaliza kusugua lile yai la bundi kwenye tumbo la Yule mama. Akacheka sana ( Kicheko cha kichawi ) Halafu akachukua yai la kuku wa kienyeji, akaliweka karibu na mdomo na kulisemesha kwa kama dakika tatu halafu akalisugua tena kwenye tumbo la Yule mama kwa dakika kadhaa, baada ya hapo akalipasua kwennye chungu..


Mungu wa kabili alisema, lengo lake lilikuwa ni kutaka kujua hiyo mimba ni ya jinsia gani, pili ni ya watoto wangapi, na tatu ni je mwanamke huyo atajifungua salama au.


Mungu wa kabili alisema, kabla haujaitoa mimba ya mtu, inabidi ujue kwanza mimba hiyo ni jinsia gani, na je ni ya mtoto mmoja au mapacha.


Mungu wa kabili akasema, ukitaka kujua kama mimba ni ya mtoto mmoja, baada ya kufanya tambiko hilo nililo lionyesha hapo juu, utapasua yai kwenye chungu cheusi na kisha.


Katika chungu hicho, kiini cha njano kikiwa kikubwa peke yake, basi atajifungua mtoto mmoja, vikiwa viini viwili, basi watoto mapacha, kama ni mtoto wa kiume, kuna herufi Fulani utaiona hapo, na kama ni wa kike, pia kuna herufi utaiona, na kama ukiona kuna damu damu, basi jua wakati wa kujifungua, eidha mtoto atakufa na mama atapona, au mtoto atapona na mama atakufa, au wote watakufa.


Majibu hayo ndio yatakayo kuongoza katika kufanya maamuzi ya kutoa au kutotoa mimba.


Mungu wa kabili akaniambia, kuna herufi Fulani, ukiiona basi kamwe usijaribu kutoa hiyo mimba, hata kwa gharama yoyote. Kwa sababu ukijaribu kufanya hivyo, jambo baya sana litatokea katika maisha yako….


Kwa bahati nzuri


UNAJUA TULIONA NINI KWENYE HILO YAI? FUATILIA SIMULIZI LANGU HAPA HAPA, SIKU YA KESHO. NITAELEZEA KITU GANI KILITOKEA. PIA NITAKUWA NIKIWEKA USHUHUDA WANGU HUU, KUPITIA : www. shuhudazaajabu.blogspot.com


MSISITIZO WANGU KWENU WATANZANIA WENZANGU, WAGANGA WA TUNGULI,WENGI W AO NI WACHAWI. HUYU MGANGA AITWAYE mungu wa kabili, NI MCHAWI.


NAONA WATU WENGI TENA WENGINE WASOMI, NA WENYE KAZI NA NAFASI NZURI TU WAMEKUWA WAKIMBILIA NA KUMUONA KAMA MUNGU KWAO. NAKUOMBA USIKUBALI KWENDA KWA MGANGA HUYO MCHAWI,. KWA SABABU NI WAKALA WA SHETANI.. UKIENDA KWAKE. UTAKUWA UMEJIUNGANISHA NA UTAWALA WA KUZIMU….


NAMBA ZA SIMU ZA HUYO MUNGU WA KABILI NI : 0744 000 473.


USIPIGE NAMBA HIZO TAFADHALI. NI NAMBA ZA WAKALA WA SHETANI AITWAYE MUNGU WA KABILI.


MUNGU AWALINDE NA AWAONGOZE KUTENDA YALIYO MEMA.
Advertisement

==

Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Bonyeza Like

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI