“Lazima Nioe Mungu Ameagiza”, Asema Man Fongo Na Anataraji Kufunga Ndoa Muda Wowote

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Msanii wa muziki wa Singeli Man Fongo amesema yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao wanaamini msanii wa muziki akioa lazima apotee kimuziki lakini hana jinsi ataoa tu kwa kuwa ni agizo la mwenyezi Mungu.


Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Hainaga Ushemeji’ amesema yeye atafunga ndoa muda wowote kwa kuwa ana mchumba ambaye amedumu naye kwenye mahusiano kwa miaka mitatu.

“Wapo wasanii kibao wameoa halafu wanapotea katika muziki ila kwa mimi Man Fongo na plan ya kuoa kwa sababu mimi watu wangu wa uswahilini,” alisema Man Fongo. “Watu wangu wa uswahilini ndo wamenibeba mpaka wakati huu watu wananielewa, kwa hiyo Man Fongo kuoa lazima nioe kwa sababu Mungu ameleta uharatibu huu ili tuufuate,”. 

Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Bonyeza Like

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI