Shilingi bilioni 3 zatafunwa kununulia mafuta katika 'magari hewa'

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania Luteni Kanali Mstaafu Dkt. Haroun Kondo (Kushoto)
  **
Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania imeuagiza uongozi wa shirika hilo kuwatambua na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria, wafanyakazi wake waliolisababishia shirika hilo hasara kupitia mikataba ya kilaghai pamoja na utendaji mbovu

Mwenyekiti wa Bodi hiyo Luteni Kanali Mstaafu Dkt. Haroun Kondo, ametoa agizo hilo jana wakati akitoa taarifa kuhusu utiaji saini ya makubaliano ya kiutendaji kati ya bodi ya wakurugenzi na uongozi juu wa shirika hilo kuhusu jinsi wanavyopaswa kuliendesha shirika hilo kwa faida.

Kwa mujibu wa Dkt. Kondo, ubadhirifu ndani ya shirika hilo umevuka mipaka na kamwe hauwezi kuvumilika ambapo alitaja baadhi ya mianya ya wizi kuwa ni katika uendeshaji na usimamizi wa rasilimali za shirika.

Alitolea mfano jinsi shilingi bilioni tatu zilivyotafunwa na wajanja wachache kwa kisingizio cha malipo ya mafuta kwa magari ambayo taarifa zake zinaonesha kuwa hayatembei kutokana na kuwa katika matengenezo kwa muda mrefu.

Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Bonyeza Like

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI