BREAKING NEWS: MBUNGE LEONIDAS GAMA AFARIKI DUNIA

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Dar es Salaam. Mbunge wa Songea Mjini (CCM), Leonidas Gama amefariki dunia katika Hospitali ya Peramiho.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Novemba 24,2017 mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho amethibitisha msiba huo.

“Nimepata taarifa jana usiku (Alhamisi Novemba 23,2017) kuwa Gama amefariki kwa kuugua shinikizo la damu,’’ amesema.

Mwisho amesema, “Tunawasiliana na familia ili kujua utaratibu wa mazishi. CCM tunasikitika kwa msiba huu, msiba ni wetu sote.”

Kabla ya kuwa mbunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Gama alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Pia, amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya za Muheza, Newala, Nachingwea, Mbeya na Ilala mkoani Dar es Salaam, 

 Chanzo; Mwananchi

Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Bonyeza Like

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI