TAARIFA KUHUSU NDEGE KUANGUKA NA KUUA WATU 11 ARUSHA

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Ndege ya Shirika la Coastal Aviation imeanguka jana na inasadikiwa watu 11 wamefariki dunia akiwemo rubani mmoja.

Ndege hiyo imegonga mlima huko Empakai Ngorongoro ikielekea Serengeti.

"Watu wote katika hiyo ndege wamefariki dunia miili  kumi ya marehemu imepatikana na mwili wa rubani haujapatikana mpaka sasa",kimeeleza chanzo cha habari.

 Hii ni ndege ya pili kwa kampuni hiyo kuanguka ndani kipindi cha miezi miwili.

Ndege ya kwanza aina ya Cessna Grand Caravan 5-THR, ilianguka Oktoba 25 2017.

Haya ni majina ya watu wanaodaiwa kuwa walikuwa ndani ya ndege hiyo

Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Bonyeza Like

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI