WAWILI WAFARIKI KWA KUPIGWA NA RADI WILAYANI KAHAMA MKOANI SHINYANGA

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Watu wawili wakazi wa kijiji cha Kalo kata ya Ulewe Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama BERNADETA SAMASON(49) na MUSTAPHA PASCHAL(12), wamefariki dunia baada ya kupigwa na radi wakati wa mvua zilizonyesha jana usiku.

Mume wa marehemu BERNADETA, COSMASS JOSEPH ameiambia DUNIA KIGANJANI BLOG leo kuwa tukio hilo limetokea jana saa 2:30 usiku wakati mvua inanyesha ambapo mke wake alikuwa ndani na mjukuu wake MUSTAPHA ambaye pia amefariki alikuwa akichota maji nje kwenye diaba.

Nae MABULA IDAMA mmoja wa mashuda wa tukio hilo amesema wakati mvua inanyesha alisikia mlio wa radi na baadae kilio na mayowe nyumbani kwa marehemu BERNADETA, alipokwenda alikuta kifo cha watu hao na hivyo alitoa taarifa kwa majirani wengine.

Afisa Mtendaji wa kijiji cha Kalo, PASCHAL MTAKI amethibitisha tukio hilo ambapo amesema alitoa taarifa kwa Afisa Mtendaji wa Kata ya Ulewe na baadae kituo cha polisi Bulungwa na baadae kuruhusu taratibu za mazishi kufanyika.

MTAKI amewatahadharisha wananchi kuacha tabia ya kuchota maji wakati mvua inanyesha kwani hali hiyo inahatarisha maisha yao sawa na mazingira ya tukio hilo la jana usiku.

Mvua iliyonyesha jana ilikuwa ni ya kwanza kubwa kunyesha katika kijiji hicho cha Kalo kilichopo katika Kata ya Ulewe, Halmashauri ya Ushetu tangu kuanza kwa kipindi hiki cha msimu wa mvua. 

Na Philipo Chimi - wa Duniakiganjani Blog - Kahama

Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Bonyeza Like

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI