HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA YASEMA ITAVIGAWA UPYA VIWANJA VILIVYOTOLEWA KWA WAFANYABIASHARA.

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Na Salvatory Ntandu.
KAHAMA


Halmashauri ya Mji wa KAHAMA imesema itavigawa upya viwanja viliyotolewa kwa wafanyabiasha (wamachinga) ambao hawataki kuhamia katika eneo la Mnadani ambalo limetengwa kwaajili ya biashara ya nguo za Mitumba.

Uamuzi huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, ANDERSON MSUMBA baada ya kubaini kuwapo kwa wafanyabiashara ambao wamekaidi agizo la kuhamia katika eneo hilo la Mnadani.

Amesema ofisi yake imemuagiza mwenyekiti wa wafanyabiashara hao, IDRISA KAYUMBO kuorodhesha majina ya wafanyabishara ambao hawataki kuhamia katika eneo hilo ili wafanyabiashara wengine wawezekugawiwa viwanja hivyo.

MSUMBA amefafanua kuwa soko la Machinga Katika Halmashauri hiyo litakuwa katika eneo hilo na wahataruhusiwa kuzurura ovyo mjini kwani serikali imewashawatengea eneo maalumu kwaaajili ya kufanyabiashara hiyo.

Zaidi ya viwanja 450 viligawiwa kwa wamachinga na Halmashauri hiyo mwaka huu ambapo tangu vitolewe uendelezaji wake umekuwa ukisuasua.

Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Bonyeza Like

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI