RAIA WAWILI WA BURUNDI WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MIWILI

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja


Raia wawili wa Burundi, STEVEN ELIAS (30) na IMINA NAJIRI(18) wamehukumiwa kwenda jela miaka 2 na miezi 6 au kulipa faini ya shilingi 500,000 kila mmoja kwa kosa la kuwepo nchini kinyume na sheria ya uhamiaji.

Akitoa hukumu hiyo hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya KAHAMA IMANI BATENZI, amesema ametoa hukumu hiyo baada ya washitakiwa kukiri kutenda kosa hilo mahakamani hapo.

SALUMU RASHID amesema washitakiwa wote kwa pamoja walikamatwa Februar 27 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi katika mtaa wa Shunu mjini Kahama huku vibali vyao vya kuwepo nchini vikiwa vimekwisha muda wake.

Katika shauri hilo la jinai namba 86/2018, washitakiwa wanadaiwa kutenda kosa kinyume na kifungu namba 45 cha sheria ya Uhamiaji namba 7 ya mwaka 1995 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016.

Hata hivyo washitakiwa wameshindwa kulipa faini na wameanza kutumikia vifungo vyao leo na mara baada ya kumaliza vifungo hivyo watarejeshwa nchini kwao Burundi.a

Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Bonyeza Like

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI