WANANCHI WANAOLIZUNGUKA BWAWA LA NYIHOGO KAHAMA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA BWAWANI HAPO

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja


Wananachi wanaozunguka bwawa la NYIHOGO Mjini KAHAMA Mkoani SHINYANGA wametakwa kujiepusha na shughuli zozote zinazosababisha uharibifu wa mazingira katika bwawa hilo.

Akizungumza jana na KAHAMA FM, kuelekea wiki ya Maji duniani, Mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya maji na usafi wa mazingira KAHAMA, (KUWASA) Meja Mstaafu BAHATI MATALA amesema mamlaka hiyo imeanza kudhibiti uharibifu katika bwawa hilo

MATALA amesema wananchi wanapaswa kutambua kuwa eneo hilo kwa sasa linahifadhiwa na kulindwa kwa mujibu wa sheria baada ya kuwa limekabidhiwa rasmi kwa KUWASA na kwamba mikakati mbalimbali imeanza kufanyika ikiwamo upandajiwa wa miti.

KUWASA imejidhatiti kuliboresha bwawa hilo kwa lengo la kusaidia kupata huduma ya maji hasa katika taasisi mbalimbali mjini Kahama pindi inapotokea dharua ya ukosefu wa huduma ya maji kutoka mradi wa ziwa victoria.

Wiki ya maji duniani inaanza kesho ambapo KUWASA itatoa elimu mbalimbali kwa wateja wake na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Hifadhi maji na mfumo wa kiikolojia kwa maendeleo ya jamii”

Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Bonyeza Like

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI